Maseneta badae leo wanatarajiwa kuwa na kikao maalum cha kumuapisha seneta mpya wa kaunti ya Elgeiyo marakwet William Kisang.

Seneta Kisang anaapishwa leo baada yake kushinda kura za uchaguzi mdogo wa useneta uliofanyika hivi majuzi katika kaunti ya Elgeiyo marakwet.

Bunge la seneti pia linatarajiwa kujadili msawada wa bunge la kitaifa wa mwaka wa 2022 wa kuzifanyia marekebisho sheria za tume ya uchaguzi nchini IEBC.

Mswada huo unalenga kubadilisha kamati maalum ya kuwateuwa makamishna wa IEBC.

Mswada huo vilevile unanuia kupunguza idadi ya wanachama wa tume ya huduma za umma PSC.

Bonioface Muchoki – Radio Ngoma 90.7 Fm

Leave a Comment