Mwenyekiti wa chama cha wazazi kaunti ya Transnzoia Wellington Waliaula anaeleza kusikitishwa na kile anakitaja kuingizwa ufisadi katika zoezi la kutoa nafasi za wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu wa 2023.

Kulingana na Waliaula baadhi ya wazazi wamekuwa wakiitishwa pesa kwenye baadhi ya shule za upili ili wanao wajiunge na shule hizo. Anasema shule nyingi zinazohusika na ufisadi huo ni zile za ngazi ya kitaifa.

Katika mahojiano na Radio Ngoma 90.7 Fm kwenye kipindi Cha Power Breakfast, Waliaula ameitaka serikali kupitia wizara ya elimu kuchunguza swala hilo na kuwachukulia hatua kali kisheria wahusika.

Sauti Yake Wellington Waliaula – Chair Parents Association Transnzoia County.

Kuhusu suala la wanafunzi wa gredi ya 6 kujiunga na shule za sekondari ngazi ya kwanza Waliaula anasema wazazi wengi wanapendelea wanafunzi hao waendelee na masomo yao kwenye shule za msingi.

Waliaula anasema asilimia kubwa ya wazazi wanaunga mkono mfumo wa elimu wa CBC kwa kuwa una manufaa mengi kwa wanafunzi ikilinganishwa na ule wa 8-4-4.

Hata hivyo anasema serikali inafaa kuzidi kuhamasisha wazazi kuhusiana na mtaala wa CBC ILI waufahamu Zaidi.

Ngoma News Desk

Leave a Comment