Huku zoezi la kuwaajiri walimu likiendelea kote nchini,wakaazi wa eneo la Kacheliba katika kaunti ya Pokot Magharibi wanaotafuta nafasi za ajira wamellalamikia idadi kubwa ya watu waanaofika eneo hilo kufafuta nafasi hizo kutoka maeneo mengine ya nchi.

Wakaazi hao wakiongozwa na Benard Lolem wanadai kwamba watu kutoka kaunti zingine ikiwemo Bungoma na Elgeiyo Marakwet wamefika eneo hilo kusaka nafasi hizo huku wakitaka maafisa wanaoendleza shughuli ya usajili kuhakikisha kwamba nafasi hizo zinawaendea wakaazi kabla ya kuwaajiri watu kutoka nje.

Hisia za Wakazi Wa Kacheliba – West Pokot.

Naye mbunge wa eneo hilo Tutus Lotee ameshtumu vikali hatua hiyo akisema kwamba kwa muda mrefu wakazi wa eneo hilo wamenyimwa nafasi za ajira huku watu kutoka maeneo mengine wakipewa nafasi hizo akisema kwamba kamwe hawatakubali hali hiyo kutokea katika zoezi hili.

Kwa upande wake naibu kamishna wa Kacheliba Kenneth Kiprop amewahakikishia wakaazi wa eneo hilo kwamba suala hilo litashughulikiwa akiwataka wanaotafuta nafasi hizo kuwa watulivu maafisa wa tume ya huduma kwa walimu TSC  wanaendeleza zoezi hilo kwa haki.

Na Ednah Munyei – Radio Ngoma.

Leave a Comment