Watahiniwa wapatao elfu 1,146 wamepata alama ya A kwenye mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne KCSE kulingana na matokeo yaliotangazwa na waziri wa elimu saa chache zlizopita.

Kulingana na matokeo yaliotangazwa na waziri wa elimu Ezekiel Machogu wanafunzi wengine elfu 173,345 wamepata alama wa C+huku wanafunzi elfu 522,588 wakipata alama ya D+.

Wanafunzi wengine wapatao elfu 30,822 wamepata alama ya E idadi hiyo ikipungua kwa asilimia 3.4 mwaka uliotangulia wa 2021 kutoka wanafunzi elfu 46,151.

Sauti ya Waziri Ezekiel Machogu.

Washikadau wa elimu kutoka kaunti ya Bungoma wakiongozwa na Katibu wa chama cha Walimu Kenneth Nganga wamewataka wazazi kuyakubali matokeo ya wanao na pia kuwasaidia kujiunga na vyuo vya ufundi na pia vyuo vikuu nchini.

Jumla ya Wanafunzi elfu 884,263 walifanya mtihani wa KCSE kati ya tarehe 2 na 23 mwezi disemba mwaka jana wa 2022.

Wale wanaotaka kujua matokeo yao kupitia simu unatuma ujumbe mfupi ukianza na nambari ya usajili wa mtihani au index Namba ikifuatiwa na KCSE unatuma kwa 20076.

Radio Ngoma News Desk.

Leave a Comment