Ufadhili huu wa Benki ya Equity Kupitia mpango wa Wings to Fly na Elimu Scholarships unalenga mwanafunzi yeyote aliyefanya mtihani wa kitaifa wa darasa la nane KCPE na kupata alama 280 na zaidi kutoka shule za Msingi za uma.

Benki ya Equity pia inafadhili wanafunzi wote walio na mahitaji maalum na ulemavu ambao walipata alama 280 na kwenda chini na pia wanafunzi yatima pamoja na wale kutoka kambi za wakimbizi waliopata alama 240 kwa wasichana na alama 250 kwa wavulana.

Fomu za ufadhili zinapatikana katika matawi yote ya benki ya Equity kote nchini leo jumatatu tarehe 23 januari ikiwa ndio siku ya mwisho ya kuwasilisha fomu hizo.

Benki ya Equty Pia inashirikiana kwa karibu na wizara ya elimu chini ya serikali ya kitaifa ili kufanikisha mpango wa elimu Scholarships.

Wanafunzi Wenye mahitaji maalum, Wanafunzi wenye ulemavu, Watoto Yatima, Wanafunzi kutoka kambi za wakimbizi na mitaa ya mabanda , wanafunzi wanaokabiliwa na umasikini na wale ambao wazazi wao wanaishi na ulemavu ndio wanaopewa kipao mbele kwenye mpango wa Elimu Scholarships.

Wanafunzi hao wanahitajika kuwa na alama 240 kwa wasichana na walimu 250 kwa wavulana.

Radio Ngoma news Desk.

Leave a Comment