Viongozi wa kisiasa kutoka eneo la teso kaunti ya Busia  wanafanya mashauriano ili kupanga jinsi watakavyo mpokea rais william ruto katika ziara yake ambayo imeratibiwa kufanyika kesho kutwa eneo hilo.

Wakiongozwa na Mbunge Oku Kaunya na Mary Emase viongozi hao wameahidi kuyapa kuwasilisha mahitaji ya wenyeji wa Busia Kwa rais ikiwemo kubuniwa kwa kaunti ya teso pamoja na masuala mengine muhimu yanayo husiana na jamii ya eneo hilo.

Wameahidi kufanya kazi pamoja na serikali kuu kwa manufaa ya wakaazi wa Busia kwa ujumla.

Sauti Zao Mary Emase na Okiya Omtata.

Upande wake mfalme wa jamii ya iteso aliyehudhuria kikao hicho Paul SAnde Emolot ambaye makao yake ni kutoka Uganda amezitaka serikali ya kenya na ile uganda kuhakikisha zinawaleta pamoja jamii zinazoishi mpakani na pia kuimarisha uchumi wa kikanda mpakani mwa nchi hizo mbili.

Na Antony Juma – Busia County.

Leave a Comment