Shule ya kutwa ya St Patrick’s Makunga wanajivunia kufanya VYEMA katika mtihani wa kidato cha nne KCSE  mwaka uliopita wa 2022 ambapo wanafunzi 94 kutoka shule hiyo wamefunzu kujiunga na vyuo vikuu nchini.

Kulingana na mwalimu mkuu wa shule hiyo Moses Wabwire matokeo hayo yamechochewa na ushirikiano mzuri kati ya walimu na wanafunzi, nidhamu ya hali ya juu miongoni mwa wanafunzi na pia kumaliza silabasi kwa muda unaofaa.

Wabwire ameongeza Kuwa Shule hiyo ni miongoni mwa shule ambazo zimefanya vyema zaidi kwenye mtihani wa Kitaifa wa Kidato cha Nne KCSE katika eneo la kaskazini mwa bonde la ufa.

Zaidi ya wanafunzi laki 8 walifanya mtihani wa kitaifa wa kidato cha 4 KCSE mwaka jana wa 2022 ambapo zaidi ya wanafunzi elfu 30 walipata alama ya E kulingana na matokeo yaliotangazwa na waziri wa elimu Ezekiel Machagu.

Idadi hiyo hata hivyo imetajwa kupungua ikilinganishwa na matokeo ya mwaka uliotangulia wa 2021 ambapo wanafunzi zaidi ya elfu 40 walipata alama ya E kwenye mtihani wa KCSE.

Wanafunzi wengine zaidi ya laki 5 wamepata alama ya D+ kwenye mtihani wa kitaifa wa KCSE 2022.

Na Linus Maiyo – Transnzoia County.

Leave a Comment