1: Saratani ya utotoni ni nini?

Saratani ya utotoni hutokea kwa watoto walio na umri wa chini ya miaka 18.

Kila mwaka inakadiriwa kuwa takriban watoto elfu 400 hupata ugonjwa wa saratani ya utotoni.

Saratani ya watoto hata hivyo inatibika na mara mingi huwa Ni nadra sana watoto kupata saratani, lakini ni muhimu kuitambua mapema.

Saratani ya Utotoni inapogunduliwa mapema Inatibika kupitia chemotherapy na wakati mwingine upasuaji au radiotherapy.

2.Mitazamo ya wanajamii kuhusu saratani au saratani ya utotoni inaweza kutofautiana.

Saratani ya utotoni sio laana kama inavyo chukuliwa na watu kutoka jamii mbalimbali.

Walezi wakati mwingine hutafuta huduma katika Tiba Asilia, Ziada na Tiba Mbadala (TCAM) kama vile waganga wa kienyeji lakini hii ni kwa wale wasio na ufahamu wa kutosha kuhusiana na tiba za saratani.

Ukweli ni kwamba saratani ya utotoni haiwezi kuponywa na waganga wa kienyeji bali Inaweza tu kutibiwa na mwathiriwa kupona kupitia chemotherapy ua kupitia upasuaji.

Saratani ya utotoni ni ugonjwa usioambukiza, kama vile shinikizo la damu au kisukari.

Radio Ngoma News Desk.

Leave a Comment