Watu 3 wamefariki dunia mapema leo na wengine 8 kujeruhiwa baada ya kuporomokewa na mgodi eneo la Tinderet kaunti ya Nandi.

Ripoti iliopo inasema 3 hao ambao wote ni wananaume wamefariki baada ya kufunikwa na mchanga kwenye mgodi wa dhahabu eneo hilo.

Walioshuhudia wanasema mgodi huo umeporomoka kutokana na utumizi wa vilipuzi katika mgodi mwingine uliokaribu.

Waliojeruhiwa wanatibiwa katika hospitali za Kaunti ya Nandi na uasingishu huku polisi wakiendeleza uchunguzi kuhusiana na tukio hilo.

Radio Ngoma -News Desk

Leave a Comment